HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaofuja Fedha Za Upanuzi Wa Viwanda Waonywa Na Rais.

Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kali kwa wanaofuja fedha zinazotengewa upanuzi wa viwanada nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya kufungua upya kiwanda cha maziwa cha KCC mjini Eldoret, Rais Kenyatta Amesema serikali itawakabili vilivyo wahusika.

Amesema utumizi mbaya wa fedha umechagia kufungwa viwnada vingi nchini na hali inayoathiri pato la taifa akielezea nkujitolea kwa serikali yake kufufua viwanda vingi ambavyo havihudumu kwa sasa.

Rais Kenyatta amesema jumla ya shilingi milioni 400 zimetumika huku akiwahimiza vijana kujihusisha kikamilifu na kilimo ili kuimarisha ukulima humu nchini akisema kiwanda cha KCC mjini Eldoret kina vigezo vya kushindana na viwanda vingine ulimwenguni.

Wakati huo huo amewahimiza wakenya kumchagua tena kwa muhula wa pili wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.

Show More

Related Articles