HabariPilipili FmPilipili FM News

Kenyatta Azindua Rasmi Kiwanda Cha Maziwa Cha KCC.

Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi kiwanda cha kutengeneza maziwa cha KCC mjini Eldoret hii leo.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo rais Kenyatta amesema jumla ya shilingi milioni 400 zimetumika huku akiwahimiza vijana kujihusisha kikamilifu na kilimo ili kuimarisha ukulima humu nchini akisema kiwanda cha KCC mjini Eldoret kina vigezo vya kushindana na viwanda vingine ulimwenguni.

Amesema serikali ya jubilee pia inalenga kufufua viwanda vingine ambavyo vimekuwa havitumika kwa muda mrefu ili kuhakikisha vijana wanapata ajira.

Wakati huo huo amewahimiza wakenya kumchagua tena kwa muhula wa pili wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.

Ameonga hayo wakati ameanza ziara yake katika kaunti ya Nandi hii leo.

Show More

Related Articles