Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Sonko,Shebesh na Sakaja wajipigia debe Umoja

Kinyang’anyiro cha kuwania Ugavana hapa jijini Nairobi kinazidi kuvutia hisia tofauti huku mrengo wa Jubilee ujulikanao kama team ”S”  yaani Sonko, Shebesh na Sakaja ukijizatiti kukabiliana na upande wa NASA uliotambulishwa kama team ”E” yaani Evans, Esther na Edwin .
Mirengo hii miwili inazidi kuwarai wapiga kura kuwaunga mkono wakati wa uchaguzi mkuu Agosti.
Hayo yakijiri cheche za maneno zinazidi kushamiri kwenye kampeni za mirengo hii miwili huku kila upande ukielekeza kidole cha lawama kwa mwenzake.
Hii leo team ‘S’ ilikuwa maeneo ya Umoja huku team ‘E’ ikikita kambi Karen na Kibra.

Show More

Related Articles