Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Naibu wa rais amtaka Buzeki kujiondoa, amuunga mkono Mandago

Naibu Rais William  Ruto  hii leo  ametangaza kumuunga  mkono  Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago  na kumtaka mpinzani wake  Zedekiah Bundotich almaarufu Buzeki kujiondoa.

Akiwa katika ngome yake ya kisiasa,  Ruto amesisitiza kuwa lengo lake ni kuhakikisha wagombeaji wote wa chama cha Jubilee wanaibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa Agosti nane.

Aidha aliwataka wote walioshindwa kwenye uteuzi wa mchujo wa Jubilee na sasa wanawania nyadhifa zao kama wagombea huru kujiondoa na kuwaunga mkono washindi na kufanya kazi pamoja.

Show More

Related Articles