HabariMilele FmSwahili

Bi Ida Odinga kukutana na viongozi wa NASA jijini Nairobi

Mkewe kiongozi wa upinzani Ida Odinga, anatarajiwa kukutana na kushauriana na viongozi wa muungano wa NASA hapa Nairobi kujadili kuhusu agenda ya NASA kuhusu uwakilishi akina mama. Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero anatarajiwa kuongoza ujumbe wa viongozi hao. NASA imekuwa ikisisitiza haja ya kuwajumuisha akina mama katika uongozi, kiongozi wake Raila Odinga akiahidi endapo atachaguliwa masuala ya akina mama yatapewa kipau mbele zaidi.

Show More

Related Articles