HabariMilele FmSwahili

William Ruto kuongoza kampeni za Jubilee kaunti ya Uasin Gishu

Naibu rais William Ruto kwa sasa anaongoza mkutano wa kisiasa eneo la Kapseret kaunti ya Uasin Gishu. Ruto aliwasili eneo hilo muda mfupi uliopita kuanza ziara yake kuhutubia mikutano kadhaa ya kisiasa. Aidha rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasili Chesongoch huko Marakwet east kuhutubia mkutano mwingine kabla ya kuelekea Chepkorio huko Keiyo south na Ainabkoi. Badaaye rais na naibu wake wataungana  mkutano wa pamoja eneo la ziwa Sirikwa na Kipkarren kaunti ya uasin gishu.wakiwa Uasin Gishu rais na naibu wake wanatarajiwa kukutana na gavana Jackson Mandago na mpinzani wake Zedekiah Bundotich kuwashawishi kusitisha misimo yao mikali inayotishia kusambaratisha umoja wa jubilee eneo hilo.

Show More

Related Articles