HabariMilele FmSwahili

Wagombea wa kike kupewa usalama

Akina mama wanaotafuta nyadhfa za umma watapewa usalama wa kutosha. Hakikisho hili limetolewa na idara ya usalama baada ya kuzinduliwa kwa nambari ya simu ya dharura 1195 inayowezesha wananchi kuripoti visa vya dhulma za jinsia. Akiongea kwenye uzinduzi huo, muasisi wa nambari hiyo Fanice Lisyagali amesema mojawapo ya ajenda ya nambari hiyo ni kuwapa utambulisho akina mama walioko katika uongozi na wale ambao wanatafuta nyadhfa za uongozi na haswa wakati huu wa uchaguzi. Idara ya polisi pia imesema itatoa ulinzi wa kutosha kwa akina mama wanaotafuta nafasi za kisiasa.

Show More

Related Articles