Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

IEBC yampiga marufuku Wavinya Ndeti kuwania ugavana kupitia Wiper

Chama cha Wiper kimepata pigo kuu baada ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kufutilia mbali uteuzi wa mgombea wa kiti cha ugavana kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti, huku chama hicho kikikabiliwa na kiwewe cha kukosa mgombeaji wa kiti hicho kumenyana na gavana Alfred mutua wa chama cha Maendeleo Chap Chap.
Kulingana na tume ya IEBC Wavinya Ndeti ni mwana chama wa vyama viwili vya kisiasa, yaani chama cha Uzalendo ambacho yeye ni kinara na kile cha Wiper, suala ambalo ni kinyume cha sheria kulingana na sheria kuhusu uchaguzi.
Hata hivyo, Wavinya amesema atakata rufaa kuhusiana na uamuzi huo.

Show More

Related Articles