HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi wa shule ya Consolata Mbeere Kusini waandamana

Zaidi ya wanafunzi 400 wa shule ya msingi ya Consolata huko Karaba Mbeere kusini, kaunti ya Kiambu wameandamana kulalamikia kuungwa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kufuatia amri ya mahakama. Wakiandamana na wazazi hao wanafunzi hao walisusia masomo na kuathiri shughuli za masomo kaitka shuyle jirani, wakidai mwalimu mkuu huyo Patrick Mutuku amekamatwa kwa kosa ambalo hakulifanya. Mutuku ambaye alihamishiwa shule hiyo miezi minne iliyopita, alikamatwa jana na kuhukumiwa jela siku 30 bila kupewa faini kwa kukosa kuhudhuria vikao vya mahakama ambapo shule hiyo inadaiwa kukosa kumlipa mwanakandarasi shilingi laki nne.

Show More

Related Articles