HabariMilele FmSwahili

Gavana Mandago na Oscar Sudi kuchunguzwa kwa madai ya uchochezi

Gavana wa Uasingishu Jackson Mandago na mbunge wa Kapset Oscar Sudi wanachunguzwa kwa madai uchochezi. Kulingana waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaisery amedhibitisha kuwa wawili hao watachukuliwa hatua za kisheria endapo watapatikana na hatia. Mandago na Sudi wanadaiwa kuzishututisha baadhi ya jamii kaunti ya Uasingishu kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao la sivyo zitimuliwe kutoka kaunti hiyo. kauli sawa na ya waziri Nkaisery imetolewa na mkuu wa polisi Joseph Boinet akionya kuwa polisi wamejiandaa kuwakabili wanasiasa wanaokiuka sheria za uchaguzi kabla na baada ya uchaguzi wa Agosti nane.

Show More

Related Articles