Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Rais Kenyatta awapa wahanga wa machafuko Nyamira Sh 470M

Rais Uhuru Kenyatta amekashifu vikali siasa za ukabila na migawanyiko na kuwanyoshea kidole cha lawama viongozi wa upinzani hasa muungano wa NASA, kwa kusema kuwa agenda yao ni ya kuligawanya taifa.
Kwenye siku yake ya pili maeneo ya South Nyanza, rais alitua Nyamira na kuahidi waathiriwa wa machafuko ya uchaguzi wa mwaka 2007 waliorejea makwao lakini bado ni wachochole kwamba serikali itawafidia katika kaunti zote 33 ikiwemo Nyamira na Kisii.
Anders Ihachi amekuwa kwenye msafara huo wa rais ambapo pia naibu rais William Ruto alizuru Bungoma na kukutana na rais kwenye tamati ya kampeni za Jubilee leo Kakamega.

Show More

Related Articles