HabariPilipili FmPilipili FM News

Ni Jukumu La Magavana Kuwalipa Wauguzi Yasema SRC.

Huku mgomo wa wauguzi ukiingia siku yake ya tatu hii leo, tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi nchini SRC  imepuuzilia mbali, madai kuwa imehusika na mgomo huo kwa kutotia saini mkataba wa maelewano kuhusu mishahara yao.

Mwenyekiti wa tume hiyo Sara Serem anasema tume yake imekuwa ikitoa mwelekeo kwa baraza la magavana nchini, kuhusu jinsi ya kumaliza mgogoro wa malipo ya wauguzi  ila hayo hayakuzingatiwa.

Serem amesisistiza kuwa ni jukumu la magavana kuwalipa wauguzi ikizingatiwa kuwa wizara hiyo iligatuliwa.

Hayo yakijiri Wagonjwa wa saratani kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali kushughulikia kwa haraka mgomo wa wauguzi ambao unaendelea kulemaza huduma za afya katika hospitali za umma.

Wengi wao wamedai kuhangaika  kupata huduma muhimu za ugonjwa huo ikizingatiwa kwa sasa wanalzimika kusafiri hadi Mombasa kupata huduma katika hospitali za kibinafsi.

Show More

Related Articles