MichezoPilipili FmPilipili FM News

Timu Ya Uingereza Yafanyishwa Mazoezi Na Jeshi.

Timu ya Taifa ya Uingereza imeweka kambi katika jeshi lao la ulinzi wa majini ili kujiweka fiti kwaajili ya michezo inayo ikabili kikosi hiko cha simba watatu.

Kikosi hiko kinaamini kuwa kufanya mazoezi ndani ya kambi ya jeshi lao tiifu itawaongezea hamasa na uimara ndani ya timu kuelekea mchezo wao wa Jumamosi wa kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Scotland na kisha kukutana na timu ya taifa ya Ufaransa.

Wadau wa soka nchini Uingereza walishitushwa wakati meneja wa kikosi hiko , Gareth Southgate kuamuru kambi yao ikafanyike katika kambi za mafunzo ya Comando wa jeshi huko Devon.

Wachezaji 22 wa timu ya taifa ya Uingereza ambao walikuwa mapumzikoni baada ya msimu wa ligi kumalizika walikubaliana na mawazo ya kocha wao kwa kambi ya timu hiyo ipelekwe katika kambi za Jeshi.

“Tunahitaji kuwapeleka vijana wetu katika mazingira tofauti ambayo wao hawakuyatarajia,”

“Jeshi lilisema tuwafanyie wachezaji wetu kitu ambacho kisicho tarajiwa na hiyo ilikuwa ni moja ya mtazamo wetu wa kambi”. Gareth Southgate aliliambia shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza FA.

 

 

 

 

Show More

Related Articles