MichezoPilipili FmPilipili FM News

Mashindano Ya Kitaifa Ya Shule Za Upili Yang’oa Nanga Mombasa.

 

Mashindano ya kitaifa ya shule za upili yameanza rasmi  huku timu mbali mbali kutoka kote nchini zikiwa tayari zimeanza kujibwaga viwanjani katika michezo mbali mbali.

Mabingwa watetezi kwenye mchezo wa mpira wa pete ama netiboli walianza vyema michuano hiyo kwa kuwabamiza na kuwavuruga wapinzani wao Moi Girls kutoka  kaskazini mashariki kwa alama (130-1).

Mchuano huo umesakatiwa katika dimba la shule ya mafunzo ya walimu la shanzu.

Katika soka ya wanaume ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 shule ya upili ya kakamega almaarufu the green commandos walitoka sare tasa na wenzao St Antony ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hio.

Wakati huohuo kwenye mchezo wa handiboli shule ya upili ya wasichana ya Moi Kamsinga waliitandika Utithi mabao 30-28.

Nao  St Francis kutoka kaunti ya Nandi waliitandika shule ya upili ya Wajir kwa mabao 52-1 kwenye mchezo wa handiboli ya wasichana huku wachezaji wa Wajir wakionekana kulemewa kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Michuano hio bado inaendeleo katika viwanja vya shule ya mafunzo ya walimu ya Shanzu na    shule ya upili ya  wavulana ya Shimo La Tewa.

 

 

Show More

Related Articles