HabariMilele FmSwahili

Bei ya mbolea kupungua kuanzia mwaka ujao

Bei ya mbolea itashuka hadi shilingi 1,200 kuanzia mwaka ujao. Naibu rais William Rutto anasema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wakulima kupata Mbolea kwa bei ya chini ili kuimarisha kilimo nchini. Akiwahutubia wananchi huko Kakamega ruto amesema kupunguzwa kwa bei ya bidhaa hiyo ndio suluhu kwa taifa hili kuzalisha chakula cha kutosha nchini. Aidha amesema bei ya mbegu za mahindi itapunguzwa kutoka shilingi 180 hadi shilingi 120 kuhakikisha wakulima wanapata bidhaa hiyo kwa urahisi.

Show More

Related Articles