HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya askari 80 wa baraza la kaunti ya Nyeri wasusia kazi

Zaidi ya askari 80 wa baraza la kaunti ya Nyeri wamesusia kazi wakidai kulipwa marupurupu yao ya takriban shilingi milioni 3.6 za mazoezi waliyofanya kwa muda wa siku 30 ili kumtumbuiza rais Uhuru Kenyatta kwenye sherehe za Madaraka. Akiongea nje ya ofisi ya gavana wa kaunti hiyo Samuel Wamathai kiongozi wao Nancy Njeri amesema kuwa waliahidiwa kulipwa marupurupu yao  siku ya alhamisi wiki jana ila hilo halijafanyika kufikia sasa.

Show More

Related Articles