MichezoPilipili FmPilipili FM News

Tusker Yabanduliwa Nje Michuano Ya SpoertPesa SUPER CUP

MICHUANO ya kugombea SpoertPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, imeaanza Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, na AFC Leopards ya Kenya kutinga Nusu Fainali wote wakipita kwa Matuta baada ya Sare ndani ya Dakika 90.

Kwenye Mechi ya Kwanza hii Timu Mpya ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, Singida United, inayoongozwa na Kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm, ilitangulia kufunga Bao Dakika ya 20 kupitia Pro wao kutoka Zimbabwe Kutinyu Tafadzwa.

Lakini AFC Leopards walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Vincent Oburu.

Hadi Dakika 90 kwisha Gemu ilibaki 1-1 na ikaja Tombola ya Mikwaju Mitano ya Penati ambapo AFC Leopards walifuzu kwa Penati 5-4.

Baada ya Mechi hii wakaingia Yanga ambao walitoka 0-0 na Tusker FC ya Kenya lakini kufuzu kwa Penati 4-2 ambazo za Yanga, waliochezesha Chipukizi wengi,  zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Obrey Chirwa, Maka Edward Mwakalukwa na Said Mussa.

Tusker FC walifunga Penati 2 wakati moja ikiokolewa na Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na nyingine kutoka nje baada kuparaza Posti.

Kwenye Nusu Fainali Yanga watacheza na AFC Leopards .

 

Show More

Related Articles