HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Giza la Gaza : Makala ya upekuzi kuhusu genge hatari la Gaza

Imekuwa ni kama desturi usalama kudorora kila tunapokaribia uchaguzi nchini.
Hofu ya wakaazi wa mitaa ya Dandora na Kayole hapa jijini Nairobi inatokana na kundi hatari la Gaza, linalojumuisha vijana waliojihami kwa kila aina ya silaha.
Leo kundi hilo limemuua afisa wa polisi na kumpokonya bunduki katika eneo la Ruai.
Baadhi ya wanasiasa wamedaiwa kufadhili kundi hilo la Gaza ili kuzua hofu na taharuki hasa wakati huu wa kampeni na uchaguzi mkuu.
Mwanahabari wetu Wallah Franklin anaangazia kwa undani genge hili kwenye makala maalum, Giza la Gaza.

Show More

Related Articles