HabariPilipili FmPilipili FM News

Wauguzi Waanza Mgomo Mombasa.

Wauguzi katika hospitali za umma kaunti ya Mombasa wameungana na wenzao wa kitaifa kuanza mgomo rasmi hii leo.

 Akiongea na waadishi wa habari katibu mkuu wa chama cha wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko amesema wamewaamuru wauguzi kaunti ya Mombasa kutofika kazini hadi pale chama hicho kitakapotoa mwelekeo rasmi.

Wamelaumu serikali za kaunti kwa kutoheshimu mkataba wao wa maelewano CBA.

Haya yanajiri huku baraza la magavana likitarajiwa kutoa taarifa kuhusiana na mgomo huo.

Baraza hilo linatarajiwa kuelezea mtazamo wale kuhusiana na mkataba wa maelewano CBA na muungano wa wauguzi nchini uliokamilishwa mapema mwaka huu lakini bado haujatiwa saini.

Wauguzi wasipungua elfu 25 wameanza mgomo huo kote nchini hii leo.

Show More

Related Articles