HabariMilele FmSwahili

Real Madrid watwaa ubingwa ulaya

Klabu ya Real Madrid ya Uhispania iliicharaza Juventus ya Italia magoli 4-1 na kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya.Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, la kwanza mnamo dakika ya 20 na lake la pili na la tatu  kwa klabu dakika ya 64 kutoka kwa krosi aliyopokezwa na  Luka Modric.

Casemiro aliwafungia Real bao lao la pili dakika ya 61 kabla ya Marco Asensio kukamilisha ushindi wao dakika ya 90 kwa bao lao la nne.Goli la kipekee la juventus lilitiwa kimiani na mchezaji Mario Mandzukic mnamo dakika ya 27.

Real Madrid wamefanikiwa kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan mwaka (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya misimu miwili mfululizo, na ni mara yao ya 12 kushinda kombe hilo.

Show More

Related Articles