HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Aisuta NASA.

Rais Uhuru Kenyatta ameusuta upinzani akiushutumu kwa kuiga mipango ya jubilee ya kutekeleza elimu ya bila malipo kwa shule za upili ifikapo mwaka ujao.

Rais Kenyatta na naibu wake wamemtaja kinara wa Upinzani Raila Odinga kama mwenye kuiga tuu kwani hawezi kuja na ajenda muhimu kwa taifa hili.

Wakati huo huo rais Kenyatta amehakikishia sekta ya usafiri wa umma kuwa kazi zao hazitoathirika kufuatia uzinduzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Amesema ujio wa reli hiyo utatoa nafasi zaidi za kazi kwa sekta ya matatu akisema ameagiza wizara ya uchukuzi kuweka vituo vya matatu katika kila kituo cha SGR ili kurahisisha usafiri.

Ameongea haya alipomaliza ziara yake ya siku tatu katika kaunti za Laikipia, nakuru na Nyandarua.

Show More

Related Articles