HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mume asakwa baada ya miili ya mkewe na wanawe kupatikana

Polisi katika eneo bunge la Kabete kaunti ya Kiambu wanamsaka mwanamume mmoja anayesemekana kuwa mhudumu wa matatu, ambaye ndiye mshukiwa mkuu katika mauaji ya watoto wake wawili na mkewe.
Haya yalibainika, baada ya wenyeji kuvunja nyumbani mwa mshukiwa kufuatia uvundo uliokithiri katika mtaa huo, na kuipata miili ya watatu hao, imelala hoi chumbani mwao.
Kwa sasa jamaa hajulikani aliko, huku uchunguzi ukianzishwa.

Show More

Related Articles