HabariPilipili FmPilipili FM News

IEBC Yamuidhinisha Shahbal Mombasa.

Mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal na mgombea mwenza wake Annania Mwaboza wameidhinishwa rasmi na tume huru ya uchaguzi na mipaka kugombania kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa.

Mara tu baada ya kuidhinishwa Shahbal amemkashifu mpinzani wake mkuu ambaye ndiye gavana wa sasa Ali Hassan Joho akisema hapaswi kupinga mradi wa reli ya kisasa akisema yeye mwenyewe wakati akiwa waziri msaidizi wa uchukuzi aliuunga mkono hivyo hapaswi kujitokeza na kuanza kulaumu mradi huo

Wakati huohuo shahbal amedokeza kuwa yuko tayarai kuhakikisha anampeleka gavana Joho Nyumbani na kubadilisha uongozi alioutaja wa kiimla

Hata hivyo shughuli ya kuidhinishwa kwa Shahbal kulichelewa kwa muda baada ya mgombea mwenza wake Annania Mwaboza kuchelewa kufika kwa kile kilichodaiwa kuwa alikua ameenda hospitali baada ya kushingwa na homa gafla

Lakini hata hivyo shughuli iliendelea baada ya yeye kufika na msimamizi wa IEBC katika kaunti ya Mombasa Nancy Kariuki akawaidhinisha rasmi.

Show More

Related Articles