BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Si Hitaji Radio Asema Msanii Papa.

Huku msimu wa siasa ukishika kasi nchini Kenya wasanii wengi wanapigania kuhusishwa kwenye kampeni hizo na wanasisasa ili kupata donge nono

Katika kaunti ya Kilifi msanii Papa almaarufu Agiza nitakuja lipa ni mmoja ya wasanii katika kaunti hio ambaye amenufaika na siasa hizo kufikia sasa na ameapa kabisa hataki maswala ya radio kwani kwa sasa yuko high season na anashukuru kwa anachokipata kutokana na hela ya siasa.

Akiongea na meza ya soga za usanii msanii huyo ameweka wazi kuwa kwa sasa hahitaji radio kwani anatosheka kwa msimu huu wa mihemko ya kisiasa.

“Kweli mimi niko high season na nashukuru si hitaji radio mpaka siasa ziishe then ntarudi kutafuta usaidizi wa maradio “. Amesema Papa.

Swala hilo limeonekana kuwakera baadhi ya wasanii kutoka pwani mwa Kenya na hata wakuu wa maradio wakiichukulia kauli ya msanii huyo kama dharau na yenye kiburi.

Kuhusiana na swala la kununua gari msanii huyo amesema ni kweli amenunua gari kutokana na malipo ya kazi ya kampeni.

Mara nyingi wasanii ikifikia wakati wa siasa hukumbatia msimu huo kwa kujiingiza kwenye mirengo ya kisiasa ili kutunga nyimbo zinazo wasifu wanasisa na kwa sababu hio wao hunufaika kwa kupata mapato mazuri.

 

Show More

Related Articles