HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Taita Wahimizwa Kuzingatia Maombi Msimu Huu Wa Siasa.

Mwakilishi wa kinamama kaunti ya Taita Taveta JOYCE LAY amewataka viongozi na jamii kwa jumla kumtanguliza Mungu kila wakati katika maisha yao hasa msimu huu wa siasa.

Akizungumza mjini WUNDANYI  alipoongoza wananchi katika maombi maalum ya kuombea kaunti hiyo na taifa hili kwa jumla, Lay amewakashifu wanaotumia nguvu za giza ili kupata uongozi.

Amewaomba wananchi kumuunga mkono na kumchagua kama seneta wao wa pili kwenye uchaguzi mkuu wa agosti.

Show More

Related Articles