HabariPilipili FmPilipili FM News

Kauli Ya Gavana Joho Kuhusu SGR.

Gavana wa kaunti ya Mombasa  Hassan Ali Joho ametishia kwenda mahakamani kuisimamisha bandari ya Mombasa dhidi ya kuweka saini ya makubaliono kuhusiana na  kulipa deni la mkopo wa shilingi  bilioni 400 pesa zilizotumiaka katika ujenzi wa reli ya kisasa.

Joho amezungumza haya masaa machache tu baada ya kuzuiliwa kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa reli ya kisasa uliofanyika asubuhi ya leo eneo la Miritini kaunti ya Mombasa,ambapo amesema deni hilo linapaswa kulipwa na shirika la reli nchini na sio bandari kupewa mzigo huo.

Joho aidha ameitaka serikali kuja na njia mbadala kwa wafanyikazi ambao wamekuwa wakitumia barabara kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Mobmasa hadi maeneo mengine akidai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wao kupoteza ajira.

 

 

 

 

 

 

Show More

Related Articles