HabariMilele FmSwahili

Peter Kenneth amteua Dan Shikanda kuwa mgombea mweza wake

Mgombea huru wa ugavana kaunti ya Nairobi Peter Kenneth amemteuwa Dan Shikanda kama mgombea mwenza wake. Kenneth anasema Shikanda ambaye amewahi hudumu kama mwenyekiti wa shirikisho la kandanda tawi la Nairobi ana ufahamu tosha kuhusu kaunti hii hasaa maswala ya vijana. Mwingine aliyemtangaza mgombea mwenza wake ni Paul Otuoma anaywewania ugavana Busia kama mgombea huru. Otuoma amemtaja Samuel Abwaku kama atakayemsaidia kubadilisha hadhi ya kaunti hiyo.

Show More

Related Articles