HabariPilipili FmPilipili FM News

NCIC Yabaini Silaha Zaingizwa Nchini Kiholela.

Tume ya uiano na utanganamo nchini NCIC imebaini kuwa kuna silaha zinazoingizwa humu nchini kutoka nchi jirani ya somalia , ambazo huenda zikatumiwa kutatiza usalama wa nchi msimu huu ambapo taifa linaelekea kwa uchaguzi.

Kamishna katika tume hiyo Morris Dzoro anasema silaha hizo huingizwa nchini kimagendo kwa hufichwa ndani ya nyama ya ng’ombe.

Dzoro amewataka wakenya kuwa makini na kuwachunguza kwa makini wageni  wote wanaoingia nchini kutoka  Somali ili kuzuia hali inayoweza kutatiza usalama wa nchi.

Show More

Related Articles