HabariMilele FmSwahili

Kenya yadhimisha siku ya kudhibiti matumizi ya tumbaku ulimwenguni leo

Kenya inaungana na ulimwengu leo kuadhimisha siku ya kudhibiti matumizi ya tumbaku ulimwenguni. Maadhimisho hufanyika kila mwaka kuangazia athari za matumizi ya tumbaku na kushinikiza kuwekwa sera mwafaka za kupunguza matumizi ya bidhaa za tumbaku. Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu tumbaku tishio kwa maendeleo. Inakisiwa kuwa nchini kenya sigara milioni 22 huvutwa kila siku hali inayochagia ongezeko la athari zake kwa wakenya.

Show More

Related Articles