HabariMilele FmSwahili

Swazuri apuuzilia mbali uwepo wa ufisadi katika mradi wa reli ya kisasa

Tume ya kitaifa ya ardhi imepuuza madai ya kuwepo ufisadi katika mradi ya reli ya kisasa inayotarajiwa kuzinduliwa kesho na rais Uhuru Kenyatta. Mwenyekiti wa NLC Mohamed Swazuri amewataja wanaoeneza madai hayo kuwa wenye nia mbaya. Pia amepinga madai kuwa mamilioni ya fedha zilipatikana nyumbani kwake wakati wa msako ulioendeshwa na makachero wa tume ya kupambana na ufisadi EACC . Wakati uo huo gharama ya usafiri katika reli ya kisasa imewekwa wazi huku wanaotaka kusafiri katika first class wakitarajiwa kulipa nauli ya shilingi 3000 nao wanaosafiri katika kiwango cha kawaida wakilipia shilingi 900.

Show More

Related Articles