HabariPilipili FmPilipili FM News

Hamu Ya Wazee Kupata Pesa Za Wazee Kinango.

Zaidi ya wazee 100 wanaostahili kupata pesa za uzeeni wanahangaika kwa  wiki moja kufikia sasa baada ya mtambo wa kutoa fedha  kukwama katika tawi la benki ya KCB huko Kinango kaunti ya Kwale.

Wazee hao wanadai wasimamizi wa tawi la benki hiyo wanasema mitambo yao imekwama na kwamba inaendelea kufanyiwa ukarabati.

Msemaji wa wazee hao  Francis Nzau  anasema wamekabiliwa na tatizo hilo kuanzia Jumatano juma lililopita.

Baadhi ya wazee hao  wamelaumu wasimamizi wa pesa hizo kwa madai ya kuzembea katika majukumu yao, wakiitaka serikali kuingilia kati na kuweka utaratibu ili waweze kupata pesa zao kwa urahisi .

Show More

Related Articles