HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Elimu ya chekechea yaathirika Ganze kufuatia ukame

Maeneo mengi humu nchi yaliathirika pakubwa  na  ukame. Moja  kati  ya  maeneo  hayo  ni  eneo  la  Ganze kaunti  ya  Kilifi.

Kuna  kikundi  maalum  kilichoathiriwa   pakubwa  na  janga la  njaa  eneo  la  Ganze nacho  ni  watoto  wa  Chekechea.

Kuanzia Januari mwaka huu hadi mwezi wa  Aprili  idadi  ya  wanafunzi  wa  Chekechea  wanaofika  shuleni, ilipungua  kwa  kiwango  kikubwa kwani  wengi  hawana  uwezo  wa  kustahimi  makali  ya  njaa, hivyo basi kuathiri elimu.

Haya yamejiri huku Waziri wa Elimu Fred Matiang’i akitangaza serikali itashika usukani wa suala la lishe shuleni kuanzia mwaka ujao.

Show More

Related Articles