HabariMilele FmSwahili

Gavana Ojaamong aikashifu tume ya EACC

Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojaamong ameikashifu tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kwa madai ya kupanga njama ya kuzuia baadhi ya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuwania nyadhifa mbalimbali kwa madia ya ufisadi au matumizi mabaya ya mamlaka dhidi yao. Akiongea kwenye hafla moja katika eneo bunge la Nambale,Ojaamong amesema tume EACC imekuwa imezembea kazini na hamna haja ya kuanza kuandama viongozi wakati huu wa uchaguzi badala yake wananchi wenye wataamua viongozi wanaotaka.

Show More

Related Articles