HabariMilele FmSwahili

Polisi 2 waaga dunia baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi

Polisi wawili wanaripotiwa kuuwawa kaunti ya Garisa mapema leo. Ni baada ya gari walimokua wakisafiria kukanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetengwa ardhini. Hiki ni kisa cha tatu cha maafisa kuuwawa eneo la Kaskazini mashariki ambapo kwa muda wa siku tatu zilizopita zaidi ya polisi 14 wanaripotiwa kuuwawa. Ni mashambulizi ambayo mshirikishi wa usalama kanda ya kaskazini mashariki Mohammud Saleh anasema yanatekelezwa na watu wanaoshirikiana na wanamgambo wa kundi la AlShaabab.

Show More

Related Articles