HabariMilele FmSwahili

NASA kuandaa mkutano jijini Nairobi wikendi hii

Muungano wa NASA umepanga msururu wa mikutano ya hadhara hapa jijini Nairobi kuanzia wikendi hii. Gavana wa Nairobi Evans Kidero ametangaza kuwa kinara wa NASA Raila Odinga ataongoza  mkutano katika eneo la Jakaranda mtaani Embakasi baada ya kuwasilisha stakabadhi za kuwania urais kwa tume ya IEBC mnamo siku ya jumapili. Kidero amedokeza kuwa NASA utalenga kura milioni moja katika kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mkuu ujao.

Show More

Related Articles