HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta aelekea Italia kuhudhuria kongamano la G7

Rais Uhuru Kenyatta ameondoka nchini leo  kuelekea nchini Italia kuhudhuria kongamano la kundi la nchi saba zinazoendelea kiviwanda maarufu kama G7 rais Kenyatta ni mmoja kati ya viongozi wanne wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo wakiwemo pia viongozi wa Ethiopia, Tunisia na Nigeria. Rais ameratibiwa kutoa hotuba kuhusiana na maendeleo ya kiteknolojia barani Afrika. Mkutano huo utahudhuriwa na rais Donald Trump wa Marekani, waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kansela wa Ujerumani Angela Merkel,waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na mwenzake wa Italia Paolo Gentiloni.

Show More

Related Articles