HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Afya Yatoa Tahadhari Ya Mkurupuko Wa Kipindipindu.

Wizara ya afya nchini imetoa tahadhari ya mkurupuko wa ugonjwa kipindupindu humu nchini.

Taarifa kutoka kwa wizara hiyo imedokeza kuwa visa 146 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kufikia sasa huku watu 4 tayari wakiwa wamepoteza maisha.

Kaunti ya Garissa inaongoza kwa visa 88, ikifuatiwa na Nairobi kwa visa 29, Vihiga visa 15, Muranga 11, Mombasa visa 2 na kaunti ya Kiambu ikiripoti kisa kimoja cha ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa huduma za afya nchini Jackson Kioko amezitaka serikali za kaunti kuweka mikakati ya kiafya, ili kusaidia kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Show More

Related Articles