MichezoPilipili FmPilipili FM News

Msnchester United Bingwa Wa Europa.

MANCHESTER UNITED huko Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden wamebeba Kombe la UEFA EUROPA LIGI baada ya kuichapa Ajax Amsterdam 2-0 katika Fainali.

Hili ni Taji la 3 kwa Man United kulitwaa Msimu huu chini ya Meneja Jose Mourinho ambae yupo Msimu wa kwanza tu na Klabu hiyo wakitwaa Ngao ya Jamii, EFL CUP na sasa UEFA EUROPA LIGI Kombe pekee la Ulaya ambalo walikuwa hawajawahi kulitwaa katika Historia yao ya kubeba Makombe Ulaya.

Kwa Jose Mourinho, ambae ametinga Fainali kubwa 14, sasa ameshinda 12 kati ya hizo.

Licha kumalixza Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kukosa nafasi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa nafasi hiyo, Ubingwa huu wa UEFA EUROPA LIGI umewapa fursa ya kutinga na kucheza Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Sasa Man United wataungana na Mabingwa wa England Chelsea, Tottenham na Man City kucheza Hatua ya Makundi ya UCL na Liverpool, ambao walimaliza Nafasi ya 4 kwenye EPL, wataanza Mechi za Mchujo ya Mashindano hayo na wakifuzu ndio watatinga Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Mechi hii imekuja Siku 2 tu tangu Mlipuko wa Jijini Manchester ulioua Watu 22 na tukio hili limeifanya Man United kuvaa Utepe Mweusi Mkononi ikiwa ni ishara ya Msiba huo.

Pia, Uwanjani, kabla Mechi kuanza, kila Mtu alisimama Dakika 1 kimya kuomboleza.

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 18 baada ya Marouane Fellaini kupewa Mpira waliounasa kutoka Mpira wa kurusha wa Ajax na kumpasia Paul Pogba ambae Shuti lake la chini lilimparaza Sanchez na kumhadaa Kipa Onana na kutinga.

Hadi Mapumziko, Ajax 0 Man United 1.

Dakika ya 48, Kona ya Juan Mata ikakutana na Kichwa cha Chris Smalling na Mpira kumfikia Henrikh Mkhitaryan ambae alikuwa kalipa mgongo Goli lakini akafunga kistaili ya Tikitaka nusu.

Show More

Related Articles