Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wabunge waidhinisha ripoti ya kumzuia Waiguru asiwanie ugavana

Takriban viongozi ishirini wa kisiasa wakiwemo wanaohudumu kwa sasa na ambao wanapania kuchaguliwa tena Agosti nane wametajwa kama ambao hawafai kuongoza.
Mashirika ya kijamii yaliyowasilisha orodha hiyo chini ya mwavuli wa the National Integrity Alliance yaliashiria kwamba viongozi hao wakiwemo magavana Evans Kidero wa Nairobi, Hassan Joho wa Mombasa na Alfred Mutua wa Machakos miongoni mwa wengine hawafai kuwa debeni.
Haya yakijiri bunge la kitaifa limeidhinisha ripoti ya kamati ya uhasibu PAC iliyompiga kumbo aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru kwa kupendekeza asiwanie afisi yoyote ya umma kutokana na sakata ya NYS.

Show More

Related Articles