HabariPilipili FmPilipili FM News

Polisi Watatu Wameuawa Baada Ya Gari Lao Kukanyaga Kilipuzi Liboi.

Maafisa watatu wa polisi wameuwawa baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi huko Liboi kaunti ya Garissa alfajiri ya leo ikiwa ni siku moja tu baada ya makao makuu ya polisi kuonya dhidi ya mashambulizi.

kulingana na ripoti ya  polisi  Maafisa hao wa utawala walikuwa wakielekea mji wa Garissa wakati tukio hilo lilipotokea katika eneo la Kulan.

Shambulio hilo limejiri baada ya inspekta generali wa polisi Joseph Boinet kuonya kuwa kundi la Al Shabaab linapanga kufanya mashambulizi nchini hususan maeneo ya mipakani.

Kulingana na idara ya ujasusi ya polisi,washambuliaji hao wamejigawa kwenye vikundi vidogo vidogo kwenye mipaka ya mji wa Mandera ambapo visa vingi vimeripotiwa vya utovu wa usalama ambapo juma lililopita watu wanne pamoja na chifu waliuawa.

Show More

Related Articles