HabariMilele FmSwahili

NTSA na KEBS zazindua mkakati wa kuzuia vifo barabarani

Mamlaka ya uchukuzi  na usalama  barabarani NTSA kwa ushirikiano na shirika la kukadiria ubora wa bidhaa KEBS zimezindua utaratibu wa ujenzi wa mabasi ya usafiri wa umma kuhakikisha kuwa endapo kunatokea ajali itapunguza vifo. Hii ni baada ya utafiti kuonyesha kwamba asilimia kubwa ya ajali zinaozohusisha matatu zinatokana na muundo usiofaa wa magari ya usafiri. Kulingana na sheria hiyo magari ya usafiri haswa matatu ya abiria kumi na zaidi yanapaswa kuweka vichuma maalum vya kuyakinga dhidi ya kuanguka. mhanidisi Gerald Wangai ni mkuu wa kitengo cha kukagua magari kaitka NTSA. Sheria hii hata hivyo inalenga magari mapya pekee huku ya sasa yakitakiwa kupewa muda wa kuimarisha udhabiti wake kuambatana na utaratibu wa NTSA.

Show More

Related Articles