HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Elfu 10 Wapandishwa Vyeo.

Jumla ya walimu elfu 10 wamepandishwa vyeo na tume ya kuajiri walimu nchini TSC baada ya mahojiano kufanywa mnamo mwezi machi na Aprili mwaka huu.

Kwenye taarifa yake TSC imesema tarehe rasmi ya kupandishwa vyeo kwao ilikuwa tarehe 3 ya mwezi huu wa mei.

TSC imesema barua za walimu waliofaulu zitatolewa na wakurugenzi wa TSC katika kila kaunti kaunzia hii leo.

Walimu hao ni miongoni mwa walimu elfu 27 waliohojiwa na TSC mwezi februari katika maeneo tofauti ya nchi.

 

Show More

Related Articles