HabariMilele FmSwahili

Watoto 3 wa muaniaji wa kisiasa Uasingishu wapatikana wamefariki

Watoto 3 wa muaniaji wadi ya Kipsoya UasinGishu James Ratemo waliotekwa nyara wamefariki. Miili ya 3 hao imepatikana ikielea katika mto nzoia huko kitale.Peter Lukoye mjomba wa watoto hao anasema kwa sasa miili hiyo inahifadhiwa katika chumba cha maiti cha Kitale ikisubiri kusafirishwa hadi Eldoret.W atoto hao walitekwa nyara na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita wakitoka kanisani. Polisi wanaendeleza uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Show More

Related Articles