HabariMilele FmSwahili

Tahadhari yatolewa kufuatia ongezeko la visa vya malaria Bomet

Tahadhari imetolewa kufuatia ongezeko la visa vya malaria katika kaunti ya Bomet katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Mkuu wa matibabu katika hospitali ya Longisa Ronny Kibet amehusisha hali hiyo na mvua inayoendelea, akisema wamewapokea zaidi ya wagonjwa 200. Kibet amedokeza kuwa 80 kati yao ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, wengine wakiwa watu wazima. Kibet kadhalika amewakumbusha wenyeji kulala ndani ya neti iliyotibiwa, kuondoa maji yaliyokwama karibu na makaazi yao na kutafuta matibabu punde wanaposhuhidia dalili za ugonjwa huo.

Show More

Related Articles