HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Mombasa Waridhishwa Na Bei Mpya Ya Unga Wa Mahindi.

Maduka mengi ya jumla hapa mjini Mombasa kufikia sasa bado hayajaanza kuuza unga kwa shilingi 90 licha ya kuagizwa na serikali kufanya hivyo.

Kufikia hii leo ni duka la jumla la Budget ambalo unga wenye nembo ya  Dola na Taifa unauzwa kwa shilingi 90 kwa paketi la kilo mbili, na shilingi 47 kwa paketi la kilo moja.

Wananchi waliofika katika duka hilo kununua unga na ambao wamedai kutoka sehemu za mbali na mji wa Mombasa, wameonyesha kuridhishwa na bei nafuu ya bidhaa hiyo, hali iliyolazimu baadhi yao kununua kwa wingi wakihofia kwamba huenda bei ikapanda tena.

Wameitaka serikali kuangazia  bei za bidhaa nyingine kama vile sukari na maziwa ambazo bei zake bado ziku juu zaidi kwa mwananchi wa pato la chini.

Show More

Related Articles