HabariPilipili FmPilipili FM News

Wafuasi Sugu Wa Wakali Kwanza Wauawa Mombasa.

Watu wanne wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi haramu la wakali kwanza eneo la Kisauni wanadaiwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi,huku watatu wakiuwawa usiku wa kuamkia leo, na mmoja akipigwa risasi asubuhi ya leo.

Wakazi eneo hilo wanasema waliouwawa ni majambazi sugu wa kundi hilo ambao wamekuwa wakiwahangaisha wananchi.

Wameitaka serikali kutuma maafisa zaidi wa polisi kushika doria katika mitaa ya kisauni,kutokana na hofu kwamba huenda kundi hilo likalipiza kisasi kwa wananchi wasiokuwa na hatia.

Juhudi zetu za kuwasiliana na afisa mkuu wa polisi eneo hilo hazikufaulu.

Show More

Related Articles