Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Nkaissery aonya mirengo mikuu dhidi ya kujitabiria ushindi

Waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaiserry ametishia kuishinikiza tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, kutowaruhusu wanasiasa wanaoeneza matamshi ya chuki na uongo miongoni mwa wakenya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Nkaissery , ambaye alikuwa akihudhuria kongamano la kimataifa kuhusu amani , amewataka wanasiasa kukoma kutabiri kuhusu idadi ya wapiga kura wanaowaunga mkono , kwani hesabu hizo hazina msingi.
Usemi wake umeungwa mkono na mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya uwiano na maridhiano Francis Ole Kaparo.

Show More

Related Articles