HabariPilipili FmPilipili FM News

Kongamano La Jumuiya Ya Pwani Lafunguliwa Rasmi Mombasa.

Magavana wa jumuiya ya kaunti za pwani wanakongamana hapa Mombasa kuweka mikakati jinsi ya kuboresha uchumi wa kikanda pwani.

Kati ya mambo yanayojadiliwa katika mkutano huo ni jinsi ya kuunda soko la kikanda, kurahisisha usafrishaji wa bidhaa kutoka kaunti moja hadi nyingine, pamoja na kuboresha soko kwa bidhaa zinazopatikana katika kaunti za  pwani.

Akiongea wakati wa kufungua rasmi kongamano hilo gavana wa Mombasa Hassan Joho, amewahimiza magavana wenza kuwekeza katika kaunti ya Mombasa, hiyo ikiwa kama njia moja ya kuinua uchumi wa kaunti.

Show More

Related Articles