BiasharaMilele FmSwahili

Benki ya Standard Chartered kutoa huduma zake kwa video na mazungumzo ya mtandaoni.

Benki ya Standard Chartered imeanza kutoa huduma zake kwa video na mazungumzo ya mtandaoni.Huduma hiyo inawapa nafasi wateja wa benki hiyo kuwasiliana na maajenti wake kwa kutumia video ya kimtandao, au mazungumzo ya kimtandao (chat). Usalama wa huduma hizo umeimarishwa ili kuwawezesha wateja kutokuwa na hofu wanapozitumia. Benki ya Standard Chartered imewekeza Dola 1.5 bilioni katika teknolojia na uzinduzi wa huduma hiyo ulikuwa katika mpango huo, alisema Mkurugenzi Mkuu wa Kenya na Eneo la Afrika Mashariki, Lamin Manjang.“Benki ya Standard Chartered inazindua teknolojia mpya ili kufanya utoaji wa huduma rahisi kwa wateja wetu. Utoaji wa huduma za benki kwa njia ya video utageuza jinsi tunavyotoa huduma,” alisema Manjang.Huduma hiyo itatekelezwa kupitia kwa mtandao kwa tovuti ya benki hiyo kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.Wateja watakuwa na uwezo wa kupata fomu na stakabadhi zingine waliko kupitia kwa huduma hiyo. Mwaka jana, Standard Chartered ilitangaza kuwa ingehamishia huduma zake za uhusiano wa wateja nchini India.Wakati huo, wafanyikazi 300 walipoteza nafasi zao za kazi.

Show More

Related Articles

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker