HabariPilipili FmPilipili FM News

Wadau Wa Kupambana Na Itikadi Kali Wahimizwa Kutotegemea Sana Ufadhili Toka Nje.

Wito umetolewa kwa serikali na wadau wengine wenye lengo la kupambana na ugaidi kutotegemea ufadhili kutoka nchi za nje katika kukabiliana na hali hiyo.

Akiongea kwenye hafla ya kuzindua mwongozo wa kupambana na ugaidi hapa Mombasa,mkurugenzi mkuu wa idara ya kitaifa ya kupamba na ugaidi Martin Kimani, amesema kusubiri ufadhili kutoka mataifa ya nje kunaweza kulemaza juhudi za kufanikisha vita hivyo.

Kimani ameunga mkono wito wa kushirikishwa kina mama katika vita hivyo, akidai kuwa wao ndio wako karibu na watoto wao ambao ndio walioathirika zaidi na janga la ugaidi na hata misimamo mikali ya kidini.

 

 

Show More

Related Articles